7 Februari 2019 - 11:40
Trump adai ushindi dhidi ya Daesh

Rais Donald Trump anaashiria kundi la kigaidi la Daesh watapokonywa ardhi yote wanayoidhibiti nchini Iraq na Syria. Matamshi hayo ameyatoa katika mkutano ulioitishwa katika wizara ya mambo ya nje

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais Donald Trump anaashiria kundi la kigaidi la Daesh watapokonywa ardhi yote wanayoidhibiti nchini Iraq na Syria. Matamshi hayo ameyatoa katika mkutano ulioitishwa katika wizara ya mambo ya nje.

Rais Donald Trump amewaambia wawakilishi wa muungano wa mataifa 79 yanayoongozwa na Marekani katika kile wanachokiita kuwa ni mapambano dhidi ya  magaidi  wa Dola la Kiislam au Daesh kwamba wanamgambo hao wanadhibiti sehemu ndogo tu ya ardhi wanayodai kuwa ni ya utawala wao au Khalifa:"Wanajeshi wa Marekani, washirika wetu na vikosi vya kidemokrasi nchini Syria wameikomboa takriban ardhi yote iliyokuwa hapo awali ikidhibitiwa na Daesh nchini Syria na Iraq. Kimsingi habari hizo huenda zikatangazwa wakati wowote kutoka sasa, pengine wiki inayokuja, kwamba tunadhibiti asili mia kwa mia ya ardhi  au Khalifat. Lakini nataka kusubiri hadi tamko rasmi . Sitaki kulisema kabla."

Ukweli ni kwamba magaidi hao wameangamizwa na majeshi ya Syria yakisaidiwa na Iran na Urusi, ambapo Marekani na washirika wake kutoka nchi 79 walikuwa wakiyatia silaha makundi ya wapiganaji ili kumuondoa madarakani rais Bashar asad.

Marekani inasisitiza kuondoa majeshi yake Syria

Maafisa wa Marekani walisema kundi la kigaidi la Daesh limepoteza asili mia 99.5 ya ardhi yao na kwamba wanadhibiti chini ya kilomita za mraba 5 nchini Syria, katika vijiji vya bonde la mto Euphrates nyumba ya kambi za jeshi la Marekani.

Serikali ya Iran imesema kuwa Marekani inatakiwa iondoe majeshi yake nchini Syria, itake isitake.

Mwisho wa habari/ 291